القيامة
Al-Qiyaama
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ
Open ayah 75:1Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ
Open ayah 75:2Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ
Open ayah 75:3Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ
Open ayah 75:4Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ
Open ayah 75:5Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ
Open ayah 75:6Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ
Open ayah 75:7Basi jicho litapo dawaa,
وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ
Open ayah 75:8Na mwezi utapo patwa,
وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ
Open ayah 75:9Na likakusanywa jua na mwezi,
يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ
Open ayah 75:10Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
كَلَّا لَا وَزَرَ
Open ayah 75:11La! Hapana pa kukimbilia!
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ
Open ayah 75:12Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
Open ayah 75:13Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٞ
Open ayah 75:14Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ
Open ayah 75:15Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ
Open ayah 75:16Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ
Open ayah 75:17Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ
Open ayah 75:18Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ
Open ayah 75:19Kisha ni juu yetu kuubainisha.
كَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ
Open ayah 75:20Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ
Open ayah 75:21Na mnaacha maisha ya Akhera.
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاضِرَةٌ
Open ayah 75:22Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٞ
Open ayah 75:23Zinamwangallia Mola wao Mlezi.
وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٞ
Open ayah 75:24Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٞ
Open ayah 75:25Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ
Open ayah 75:26La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,
وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٖ
Open ayah 75:27Na pakasemwa: Nani wa kumganga?
وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ
Open ayah 75:28Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;
وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ
Open ayah 75:29Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ
Open ayah 75:30Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ
Open ayah 75:31Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.
وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Open ayah 75:32Bali alikanusha, na akageuka.
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ
Open ayah 75:33Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ
Open ayah 75:34Ole wako, ole wako!
ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ
Open ayah 75:35Kisha Ole wako, ole wako!
أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى
Open ayah 75:36Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةٗ مِّن مَّنِيّٖ يُمۡنَىٰ
Open ayah 75:37Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةٗ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ
Open ayah 75:38Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.
فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ
Open ayah 75:39Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
أَلَيۡسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰ
Open ayah 75:40Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?