المدثر
Al-Muddaththir
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُدَّثِّرُ
Open ayah 74:1Ewe uliye jigubika!
قُمۡ فَأَنذِرۡ
Open ayah 74:2Simama uonye!
وَرَبَّكَ فَكَبِّرۡ
Open ayah 74:3Na Mola wako Mlezi mtukuze!
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرۡ
Open ayah 74:4Na nguo zako, zisafishe.
وَٱلرُّجۡزَ فَٱهۡجُرۡ
Open ayah 74:5Na yaliyo machafu yahame!
وَلَا تَمۡنُن تَسۡتَكۡثِرُ
Open ayah 74:6Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.
وَلِرَبِّكَ فَٱصۡبِرۡ
Open ayah 74:7Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!
فَإِذَا نُقِرَ فِي ٱلنَّاقُورِ
Open ayah 74:8Basi litapo pulizwa barugumu,
فَذَٰلِكَ يَوۡمَئِذٖ يَوۡمٌ عَسِيرٌ
Open ayah 74:9Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.
عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ غَيۡرُ يَسِيرٖ
Open ayah 74:10Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.
ذَرۡنِي وَمَنۡ خَلَقۡتُ وَحِيدٗا
Open ayah 74:11Niache peke yangu na niliye muumba;
وَجَعَلۡتُ لَهُۥ مَالٗا مَّمۡدُودٗا
Open ayah 74:12Na nikamjaalia awe na mali mengi,
وَبَنِينَ شُهُودٗا
Open ayah 74:13Na wana wanao onekana,
وَمَهَّدتُّ لَهُۥ تَمۡهِيدٗا
Open ayah 74:14Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa.
ثُمَّ يَطۡمَعُ أَنۡ أَزِيدَ
Open ayah 74:15Kisha anatumai nimzidishie!
كَلَّآۖ إِنَّهُۥ كَانَ لِأٓيَٰتِنَا عَنِيدٗا
Open ayah 74:16Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!
سَأُرۡهِقُهُۥ صَعُودًا
Open ayah 74:17Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana.
إِنَّهُۥ فَكَّرَ وَقَدَّرَ
Open ayah 74:18Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.
فَقُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ
Open ayah 74:19Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!
ثُمَّ قُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ
Open ayah 74:20Tena ameangamia! Vipi alivyo pima!
ثُمَّ نَظَرَ
Open ayah 74:21Kisha akatazama,
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
Open ayah 74:22Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
ثُمَّ أَدۡبَرَ وَٱسۡتَكۡبَرَ
Open ayah 74:23Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
فَقَالَ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ يُؤۡثَرُ
Open ayah 74:24Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa.
إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا قَوۡلُ ٱلۡبَشَرِ
Open ayah 74:25Haya si chochote ila kauli ya binaadamu.
سَأُصۡلِيهِ سَقَرَ
Open ayah 74:26Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سَقَرُ
Open ayah 74:27Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?
لَا تُبۡقِي وَلَا تَذَرُ
Open ayah 74:28Haubakishi wala hausazi.
لَوَّاحَةٞ لِّلۡبَشَرِ
Open ayah 74:29Unababua ngozi iwe nyeusi.
عَلَيۡهَا تِسۡعَةَ عَشَرَ
Open ayah 74:30Juu yake wapo kumi na tisa.
وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَٰٓئِكَةٗۖ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَهُمۡ إِلَّا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَٰنٗا وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡكَٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ
Open ayah 74:31Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.
كَلَّا وَٱلۡقَمَرِ
Open ayah 74:32Hasha! Naapa kwa mwezi!
وَٱلَّيۡلِ إِذۡ أَدۡبَرَ
Open ayah 74:33Na kwa usiku unapo kucha!
وَٱلصُّبۡحِ إِذَآ أَسۡفَرَ
Open ayah 74:34Na kwa asubuhi inapo pambazuka!
إِنَّهَا لَإِحۡدَى ٱلۡكُبَرِ
Open ayah 74:35Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
نَذِيرٗا لِّلۡبَشَرِ
Open ayah 74:36Ni onyo kwa binaadamu,
لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَتَقَدَّمَ أَوۡ يَتَأَخَّرَ
Open ayah 74:37Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.
كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ رَهِينَةٌ
Open ayah 74:38Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma.
إِلَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡيَمِينِ
Open ayah 74:39Isipo kuwa watu wa kuliani.
فِي جَنَّٰتٖ يَتَسَآءَلُونَ
Open ayah 74:40Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
عَنِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Open ayah 74:41Khabari za wakosefu:
مَا سَلَكَكُمۡ فِي سَقَرَ
Open ayah 74:42Ni nini kilicho kupelekeni Motoni?
قَالُواْ لَمۡ نَكُ مِنَ ٱلۡمُصَلِّينَ
Open ayah 74:43Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali.
وَلَمۡ نَكُ نُطۡعِمُ ٱلۡمِسۡكِينَ
Open ayah 74:44Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.
وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلۡخَآئِضِينَ
Open ayah 74:45Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu.
وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Open ayah 74:46Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo.
حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلۡيَقِينُ
Open ayah 74:47Mpaka yakini ilipo tufikia.
فَمَا تَنفَعُهُمۡ شَفَٰعَةُ ٱلشَّٰفِعِينَ
Open ayah 74:48Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
فَمَا لَهُمۡ عَنِ ٱلتَّذۡكِرَةِ مُعۡرِضِينَ
Open ayah 74:49Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
كَأَنَّهُمۡ حُمُرٞ مُّسۡتَنفِرَةٞ
Open ayah 74:50Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,
فَرَّتۡ مِن قَسۡوَرَةِۭ
Open ayah 74:51Wanao mkimbia simba!
بَلۡ يُرِيدُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُؤۡتَىٰ صُحُفٗا مُّنَشَّرَةٗ
Open ayah 74:52Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa.
كَلَّاۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ
Open ayah 74:53Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera?
كَلَّآ إِنَّهُۥ تَذۡكِرَةٞ
Open ayah 74:54Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Open ayah 74:55Basi anaye taka atakumbuka.
وَمَا يَذۡكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ هُوَ أَهۡلُ ٱلتَّقۡوَىٰ وَأَهۡلُ ٱلۡمَغۡفِرَةِ
Open ayah 74:56Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.