المطففين
Al-Mutaffifin
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ
Open ayah 83:1Ole wao hao wapunjao!
ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ
Open ayah 83:2Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ
Open ayah 83:3Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ
Open ayah 83:4Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ
Open ayah 83:5Katika Siku iliyo kuu,
يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Open ayah 83:6Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ
Open ayah 83:7Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ
Open ayah 83:8Unajua nini Sijjin?
كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ
Open ayah 83:9Kitabu kilicho andikwa.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 83:10Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Open ayah 83:11Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ
Open ayah 83:12Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Open ayah 83:13Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Open ayah 83:14Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.
كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ
Open ayah 83:15Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ
Open ayah 83:16Kisha wataingia Motoni!
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Open ayah 83:17Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ
Open ayah 83:18Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
Open ayah 83:19Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?
كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ
Open ayah 83:20Kitabu kilicho andikwa.
يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Open ayah 83:21Wanakishuhudia walio karibishwa.
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ
Open ayah 83:22Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Open ayah 83:23Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ
Open ayah 83:24Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ
Open ayah 83:25Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ
Open ayah 83:26Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.
وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ
Open ayah 83:27Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Open ayah 83:28Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ
Open ayah 83:29Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.
وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ
Open ayah 83:30Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana.
وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ
Open ayah 83:31Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
Open ayah 83:32Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ
Open ayah 83:33Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ
Open ayah 83:34Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Open ayah 83:35Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Open ayah 83:36Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?