الإنفطار
Al-Infitaar
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ
Open ayah 82:1Mbingu itapo chanika,
وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ
Open ayah 82:2Na nyota zitapo tawanyika,
وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ
Open ayah 82:3Na bahari zitakapo pasuliwa,
وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ
Open ayah 82:4Na makaburi yatapo fukuliwa,
عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ
Open ayah 82:5Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ
Open ayah 82:6Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ
Open ayah 82:7Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ
Open ayah 82:8Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ
Open ayah 82:9Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ
Open ayah 82:10Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
كِرَامٗا كَٰتِبِينَ
Open ayah 82:11Waandishi wenye hishima,
يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ
Open ayah 82:12Wanayajua mnayo yatenda.
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٖ
Open ayah 82:13Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ
Open ayah 82:14Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Open ayah 82:15Wataingia humo Siku ya Malipo.
وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ
Open ayah 82:16Na hawatoacha kuwamo humo.
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Open ayah 82:17Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Open ayah 82:18Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ
Open ayah 82:19Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.