المرسلات
Al-Mursalaat
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا
Open ayah 77:1Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا
Open ayah 77:2Na zinazo vuma kwa kasi!
وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا
Open ayah 77:3Na zikaeneza maeneo yote!
فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا
Open ayah 77:4Na zinazo farikisha zikatawanya!
فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا
Open ayah 77:5Na zinazo peleka mawaidha!
عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا
Open ayah 77:6Kwa kuudhuru au kuonya,
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ
Open ayah 77:7Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ
Open ayah 77:8Wakati nyota zitakapo futwa,
وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ
Open ayah 77:9Na mbingu zitakapo pasuliwa,
وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ
Open ayah 77:10Na milima itakapo peperushwa,
وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ
Open ayah 77:11Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ
Open ayah 77:12Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ
Open ayah 77:13Kwa siku ya kupambanua!
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ
Open ayah 77:14Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:15Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ
Open ayah 77:16Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ
Open ayah 77:17Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ
Open ayah 77:18Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:19Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ
Open ayah 77:20Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ
Open ayah 77:21Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ
Open ayah 77:22Mpaka muda maalumu?
فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ
Open ayah 77:23Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:24Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا
Open ayah 77:25Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا
Open ayah 77:26Walio hai na maiti?
وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا
Open ayah 77:27Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:28Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Open ayah 77:29Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ
Open ayah 77:30Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ
Open ayah 77:31Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ
Open ayah 77:32Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ
Open ayah 77:33Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:34Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ
Open ayah 77:35Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ
Open ayah 77:36Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:37Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ
Open ayah 77:38Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ
Open ayah 77:39Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:40Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ
Open ayah 77:41Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ
Open ayah 77:42Na matunda wanayo yapenda,
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Open ayah 77:43Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Open ayah 77:44Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:45Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ
Open ayah 77:46Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:47Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ
Open ayah 77:48Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Open ayah 77:49Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Open ayah 77:50Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?