الحاقة
Al-Haaqqa
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱلۡحَآقَّةُ
Open ayah 69:1Tukio la haki.
مَا ٱلۡحَآقَّةُ
Open ayah 69:2Nini hilo Tukio la haki?
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ
Open ayah 69:3Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ
Open ayah 69:4Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha.
فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ
Open ayah 69:5Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.
وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ
Open ayah 69:6Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika.
سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ
Open ayah 69:7Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.
فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ
Open ayah 69:8Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki?
وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ
Open ayah 69:9Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia.
فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً
Open ayah 69:10Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ
Open ayah 69:11Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina,
لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ
Open ayah 69:12Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi.
فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ
Open ayah 69:13Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu,
وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ
Open ayah 69:14Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja,
فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Open ayah 69:15Siku hiyo ndio Tukio litatukia.
وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ
Open ayah 69:16Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.
وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ
Open ayah 69:17Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.
يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ
Open ayah 69:18Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ
Open ayah 69:19Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!
إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ
Open ayah 69:20Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.
فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ
Open ayah 69:21Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza,
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ
Open ayah 69:22Katika Bustani ya juu,
قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ
Open ayah 69:23Matunda yake yakaribu.
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ
Open ayah 69:24Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita.
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ
Open ayah 69:25Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu!
وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ
Open ayah 69:26Wala nisingeli jua nini hisabu yangu.
يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ
Open ayah 69:27Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa.
مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ
Open ayah 69:28Mali yangu hayakunifaa kitu.
هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ
Open ayah 69:29Madaraka yangu yamenipotea.
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ
Open ayah 69:30(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!
ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ
Open ayah 69:31Kisha mtupeni Motoni!
ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ
Open ayah 69:32Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!
إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ
Open ayah 69:33Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu,
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Open ayah 69:34Wala hahimizi kulisha masikini.
فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ
Open ayah 69:35Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu,
وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ
Open ayah 69:36Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ
Open ayah 69:37Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ
Open ayah 69:38Basi naapa kwa mnavyo viona,
وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ
Open ayah 69:39Na msivyo viona,
إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ
Open ayah 69:40Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.
وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ
Open ayah 69:41Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.
وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ
Open ayah 69:42Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Open ayah 69:43Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ
Open ayah 69:44Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu,
لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ
Open ayah 69:45Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia,
ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ
Open ayah 69:46Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!
فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ
Open ayah 69:47Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia.
وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ
Open ayah 69:48Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu.
وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ
Open ayah 69:49Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ
Open ayah 69:50Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.
وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ
Open ayah 69:51Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Open ayah 69:52Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.