النازعات
An-Naazi'aat
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا
Open ayah 79:1Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu,
وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا
Open ayah 79:2Na kwa wanao toa kwa upole,
وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا
Open ayah 79:3Na wanao ogelea,
فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا
Open ayah 79:4Wakishindana mbio,
فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا
Open ayah 79:5Wakidabiri mambo.
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ
Open ayah 79:6Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ
Open ayah 79:7Kifuate cha kufuatia.
قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ
Open ayah 79:8Siku hiyo nyoyo zitapiga piga,
أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ
Open ayah 79:9Macho yatainama chini.
يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ
Open ayah 79:10Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ
Open ayah 79:11Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ
Open ayah 79:12Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!
فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ
Open ayah 79:13Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ
Open ayah 79:14Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Open ayah 79:15Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى
Open ayah 79:16Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia:
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Open ayah 79:17Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
Open ayah 79:18Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ
Open ayah 79:19Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Open ayah 79:20Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
Open ayah 79:21Lakini aliikadhibisha na akaasi.
ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ
Open ayah 79:22Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
Open ayah 79:23Akakusanya watu akanadi.
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Open ayah 79:24Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ
Open ayah 79:25Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ
Open ayah 79:26Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.
ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا
Open ayah 79:27Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا
Open ayah 79:28Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا
Open ayah 79:29Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.
وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
Open ayah 79:30Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا
Open ayah 79:31Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا
Open ayah 79:32Na milima akaisimamisha,
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Open ayah 79:33Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Open ayah 79:34Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ
Open ayah 79:35Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,
وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
Open ayah 79:36Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
Open ayah 79:37Basi ama yule aliye zidi ujeuri,
وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Open ayah 79:38Na akakhiari maisha ya dunia,
فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Open ayah 79:39Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ
Open ayah 79:40Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Open ayah 79:41Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا
Open ayah 79:42Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ
Open ayah 79:43Una nini wewe hata uitaje?
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ
Open ayah 79:44Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا
Open ayah 79:45Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu.
كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا
Open ayah 79:46Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.