الفجر
Al-Fajr
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلۡفَجۡرِ
Open ayah 89:1Naapa kwa alfajiri,
وَلَيَالٍ عَشۡرٖ
Open ayah 89:2Na kwa masiku kumi,
وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ
Open ayah 89:3Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja,
وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ
Open ayah 89:4Na kwa usiku unapo pita,
هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٞ لِّذِي حِجۡرٍ
Open ayah 89:5Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ
Open ayah 89:6Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?
إِرَمَ ذَاتِ ٱلۡعِمَادِ
Open ayah 89:7Wa Iram, wenye majumba marefu?
ٱلَّتِي لَمۡ يُخۡلَقۡ مِثۡلُهَا فِي ٱلۡبِلَٰدِ
Open ayah 89:8Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?
وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ
Open ayah 89:9Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?
وَفِرۡعَوۡنَ ذِي ٱلۡأَوۡتَادِ
Open ayah 89:10Na Firauni mwenye vigingi?
ٱلَّذِينَ طَغَوۡاْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ
Open ayah 89:11Ambao walifanya jeuri katika nchi?
فَأَكۡثَرُواْ فِيهَا ٱلۡفَسَادَ
Open ayah 89:12Wakakithirisha humo ufisadi?
فَصَبَّ عَلَيۡهِمۡ رَبُّكَ سَوۡطَ عَذَابٍ
Open ayah 89:13Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.
إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلۡمِرۡصَادِ
Open ayah 89:14Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.
فَأَمَّا ٱلۡإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكۡرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَكۡرَمَنِ
Open ayah 89:15Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!
وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيۡهِ رِزۡقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَهَٰنَنِ
Open ayah 89:16Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!
كَلَّاۖ بَل لَّا تُكۡرِمُونَ ٱلۡيَتِيمَ
Open ayah 89:17Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,
وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Open ayah 89:18Wala hamhimizani kulisha masikini;
وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلٗا لَّمّٗا
Open ayah 89:19Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,
وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبّٗا جَمّٗا
Open ayah 89:20Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
كَلَّآۖ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكّٗا دَكّٗا
Open ayah 89:21Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande,
وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفّٗا صَفّٗا
Open ayah 89:22Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu,
وَجِاْيٓءَ يَوۡمَئِذِۭ بِجَهَنَّمَۚ يَوۡمَئِذٖ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكۡرَىٰ
Open ayah 89:23Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?
يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي قَدَّمۡتُ لِحَيَاتِي
Open ayah 89:24Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!
فَيَوۡمَئِذٖ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٞ
Open ayah 89:25Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.
وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٞ
Open ayah 89:26Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.
يَٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَئِنَّةُ
Open ayah 89:27Ewe nafsi iliyo tua!
ٱرۡجِعِيٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةٗ مَّرۡضِيَّةٗ
Open ayah 89:28Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.
فَٱدۡخُلِي فِي عِبَٰدِي
Open ayah 89:29Basi ingia miongoni mwa waja wangu,
وَٱدۡخُلِي جَنَّتِي
Open ayah 89:30Na ingia katika Pepo yangu.