الغاشية
Al-Ghaashiya
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ
Open ayah 88:1Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ
Open ayah 88:2Siku hiyo nyuso zitainama,
عَامِلَةٞ نَّاصِبَةٞ
Open ayah 88:3Zikifanya kazi, nazo taabani.
تَصۡلَىٰ نَارًا حَامِيَةٗ
Open ayah 88:4Ziingie katika Moto unao waka -
تُسۡقَىٰ مِنۡ عَيۡنٍ ءَانِيَةٖ
Open ayah 88:5Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
لَّيۡسَ لَهُمۡ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٖ
Open ayah 88:6Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
لَّا يُسۡمِنُ وَلَا يُغۡنِي مِن جُوعٖ
Open ayah 88:7Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاعِمَةٞ
Open ayah 88:8Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
لِّسَعۡيِهَا رَاضِيَةٞ
Open ayah 88:9Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ
Open ayah 88:10Katika Bustani ya juu.
لَّا تَسۡمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةٗ
Open ayah 88:11Hawatasikia humo upuuzi.
فِيهَا عَيۡنٞ جَارِيَةٞ
Open ayah 88:12Humo imo chemchem inayo miminika.
فِيهَا سُرُرٞ مَّرۡفُوعَةٞ
Open ayah 88:13Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
وَأَكۡوَابٞ مَّوۡضُوعَةٞ
Open ayah 88:14Na bilauri zilizo pangwa,
وَنَمَارِقُ مَصۡفُوفَةٞ
Open ayah 88:15Na matakia safu safu,
وَزَرَابِيُّ مَبۡثُوثَةٌ
Open ayah 88:16Na mazulia yaliyo tandikwa.
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ
Open ayah 88:17Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ رُفِعَتۡ
Open ayah 88:18Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
وَإِلَى ٱلۡجِبَالِ كَيۡفَ نُصِبَتۡ
Open ayah 88:19Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
وَإِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَيۡفَ سُطِحَتۡ
Open ayah 88:20Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٞ
Open ayah 88:21Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ
Open ayah 88:22Wewe si mwenye kuwatawalia.
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ
Open ayah 88:23Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَكۡبَرَ
Open ayah 88:24Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
إِنَّ إِلَيۡنَآ إِيَابَهُمۡ
Open ayah 88:25Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا حِسَابَهُم
Open ayah 88:26Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!