الأعلى
Al-A'laa
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى
Open ayah 87:1Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ
Open ayah 87:2Aliye umba, na akaweka sawa,
وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ
Open ayah 87:3Na ambaye amekadiria na akaongoa,
وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ
Open ayah 87:4Na aliye otesha malisho,
فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ
Open ayah 87:5Kisha akayafanya makavu, meusi.
سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ
Open ayah 87:6Tutakusomesha wala hutasahau,
إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ
Open ayah 87:7Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ
Open ayah 87:8Na tutakusahilishia yawe mepesi.
فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ
Open ayah 87:9Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ
Open ayah 87:10Atakumbuka mwenye kuogopa.
وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى
Open ayah 87:11Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Open ayah 87:12Ambaye atauingia Moto mkubwa.
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ
Open ayah 87:13Tena humo hatakufa wala hawi hai.
قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ
Open ayah 87:14Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ
Open ayah 87:15Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Open ayah 87:16Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ
Open ayah 87:17Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ
Open ayah 87:18Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ
Open ayah 87:19Vitabu vya Ibrahimu na Musa.