الطارق
At-Taariq
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ
Open ayah 86:1Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ
Open ayah 86:2Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ
Open ayah 86:3Ni Nyota yenye mwanga mkali.
إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ
Open ayah 86:4Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ
Open ayah 86:5Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ
Open ayah 86:6Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ
Open ayah 86:7Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ
Open ayah 86:8Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ
Open ayah 86:9Siku zitakapo dhihirishwa siri.
فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ
Open ayah 86:10Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ
Open ayah 86:11Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ
Open ayah 86:12Na kwa ardhi inayo pasuka!
إِنَّهُۥ لَقَوۡلٞ فَصۡلٞ
Open ayah 86:13Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ
Open ayah 86:14Wala si mzaha.
إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدٗا
Open ayah 86:15Hakika wao wanapanga mpango.
وَأَكِيدُ كَيۡدٗا
Open ayah 86:16Na Mimi napanga mpango.
فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا
Open ayah 86:17Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.