البروج
Al-Burooj
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ
Open ayah 85:1Naapa kwa mbingu yenye Buruji!
وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ
Open ayah 85:2Na kwa siku iliyo ahidiwa!
وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ
Open ayah 85:3Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!
قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ
Open ayah 85:4Wameangamizwa watu wa makhandaki
ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ
Open ayah 85:5Yenye moto wenye kuni nyingi,
إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ
Open ayah 85:6Walipo kuwa wamekaa hapo,
وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ
Open ayah 85:7Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini.
وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ
Open ayah 85:8Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa,
ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Open ayah 85:9Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu.
إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ
Open ayah 85:10Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ
Open ayah 85:11Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ
Open ayah 85:12Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ
Open ayah 85:13Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena,
وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ
Open ayah 85:14Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,
ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ
Open ayah 85:15Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu,
فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ
Open ayah 85:16Atendaye ayatakayo.
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ
Open ayah 85:17Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi?
فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ
Open ayah 85:18Ya Firauni na Thamudi?
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ
Open ayah 85:19Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha.
وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ
Open ayah 85:20Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.
بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ
Open ayah 85:21Bali hii ni Qur'ani tukufu
فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ
Open ayah 85:22Katika Ubao Ulio Hifadhiwa.