العاديات
Al-Aadiyaat
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحٗا
Open ayah 100:1Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحٗا
Open ayah 100:2Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحٗا
Open ayah 100:3Wakishambulia wakati wa asubuhi,
فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعٗا
Open ayah 100:4Huku wakitimua vumbi,
فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا
Open ayah 100:5Na wakijitoma kati ya kundi,
إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٞ
Open ayah 100:6Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٞ
Open ayah 100:7Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلۡخَيۡرِ لَشَدِيدٌ
Open ayah 100:8Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
۞أَفَلَا يَعۡلَمُ إِذَا بُعۡثِرَ مَا فِي ٱلۡقُبُورِ
Open ayah 100:9Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
وَحُصِّلَ مَا فِي ٱلصُّدُورِ
Open ayah 100:10Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
إِنَّ رَبَّهُم بِهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّخَبِيرُۢ
Open ayah 100:11Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!