الضحى
Ad-Dhuhaa
Translation: Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani · Open the surah
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلضُّحَىٰ
Open ayah 93:1Naapa kwa mchana!
وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ
Open ayah 93:2Na kwa usiku unapo tanda!
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
Open ayah 93:3Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ
Open ayah 93:4Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ
Open ayah 93:5Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمٗا فَـَٔاوَىٰ
Open ayah 93:6Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
وَوَجَدَكَ ضَآلّٗا فَهَدَىٰ
Open ayah 93:7Na akakukuta umepotea akakuongoa?
وَوَجَدَكَ عَآئِلٗا فَأَغۡنَىٰ
Open ayah 93:8Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ
Open ayah 93:9Basi yatima usimwonee!
وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ
Open ayah 93:10Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ
Open ayah 93:11Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.